Kyombo atua NAPSA Stars ya Zambia

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th April 2026


Kyombo atua NAPSA Stars ya Zambia

Mshambuliaji wa Tanzania Habib Kyombo amejiunga rasmi na klabu ya NAPSA Stars ya Zambia, katika uhamisho huru baada ya kuachana na klabu ya Mbeya City.

Kwa mujibu wa taarifa za usajili kutoka ndani ya klabu hiyo, Kyombo amekamilisha uhamisho wake baada ya makubaliano kufikiwa kati ya pande zote mbili, hatua inayotarajiwa kuongeza nguvu kwenye kikosi cha NAPSA Stars kuelekea msimu mpya wa ligi.

Kyombo, ambaye amewahi kucheza katika klabu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwemo Simba SC na Singida Fountain Gate, anakwenda Zambia akiwa na uzoefu wa kutosha katika ushindani wa soka la Afrika Mashariki.

Klabu hiyo ya Zambia inaendelea kufanya maboresho ya kikosi chake kwa lengo la kufanya vizuri zaidi kwenye msimamo wa ligi. Usajili wa Kyombo unaonekana kama sehemu ya mkakati wa muda mfupi na mrefu wa kuongeza ushindani ndani ya timu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.