Kiungo Coastal Union kuibukia TP Mazembe

Joel JJ By Joel JJ β€’ 30th May 2026


Kiungo Coastal Union kuibukia TP Mazembe

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Coastal Union, Bakari Msimu, amekamilisha rasmi usajili wake wa kujiunga na vigog wa soka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, TP Mazembe, katika hatua kubwa ya maendeleo ya maisha yake ya soka.

Makubaliano kati ya Coastal Union na TP Mazembe yamefikiwa kwa mafanikio, huku nyota huyo kijana akisubiri kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 kabla ya kuanza rasmi safari yake mpya nchini DR Congo.

Msimu amekuwa mmoja wa vijana wanaotajwa kuwa na mustakabali mkubwa katika soka la Tanzania kutokana na uwezo wake wa kucheza maeneo mbalimbali, kasi, ubunifu na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao.

Hatua ya kujiunga na TP Mazembe inaonekana kuwa fursa muhimu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye sasa atapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika moja ya klabu kubwa na zenye historia kubwa zaidi barani Afrika.

Msimu ni sehemu ya wachezaji walioitwa kikosi cha Taif Stars kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Rwanda na Uganda.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.