Kariakoo Derby sasa kupigwa dimba la Isamuhyo

Joel JJ By Joel JJ • 24th April 2026


Kariakoo Derby sasa kupigwa dimba la Isamuhyo

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imethibitisha mabadiliko ya uwanja kwa mchezo namba 169 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC na Yanga SC, ambao umepangwa kuchezwa tarehe 03 Mei.

Awali, mchezo huo ulitarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, sasa umehamishiwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa kwa ajili ya matengenezo.

Mchezo huo mkubwa wa “Dabi ya Kariakoo” unatarajiwa kupigwa majira ya saa 12:00 jioni.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.