Ibenge aitaka nusu fainali kombe la Muungano

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st April 2026


Ibenge aitaka nusu fainali kombe la Muungano

Kocha Mkuu wa Azam Fc Florent Ibenge amekiri kuwa mchezo wa robo fainali kombe la Muungano dhidi ya KVZ anatarajia utakuwa mgumu hata hivyo lengo lake ni kuona wanashinda mchezo huo na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Ibenge amesema KVZ ni moja ya timu bora visiwani Zanzibar ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hivyo anatarajiwa hawatakuwa na kazi nyepesi dhidi yao hapo kesho.

"Sisi tunafanya maandalizi yetu tukiwa na lengo la kushinda na kusonga mbele hatua ya nusu fainali."

"Bila ya kuwakosea heshima wapinzani wetu, natambua wana timu nzuri kwa sasa unaweza kusema ndio timu hapa visiwani Zanzibar lakini nisema tu sisi tunataka kufuzu hatua inayofuata," alisema.

Azam Fc walitua visiwani Zanzibar jana leo wakitarajiwa kukamilisha maandalizi yao tayari kwa mtanange dhidi ya KVZ ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Endapo Azam Fc itafuzu hatua ya nusu fainali, inaweza kukutana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga ambao wao wanacheza leo dhidi ya Muembe Makumbi katika mchezo wa kwanza wa robo fainali


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.