Hizi hapa mechi kubwa ligi ya Premia leo Jumamosi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th April 2026


Hizi hapa mechi kubwa ligi ya Premia leo Jumamosi

Michezo ya kusisimua ligi kuu ya Premia inatarajiwa kuchezwa leo huku ushindani ukizidi kupamba moto katika mbio za ubingwa, nafasi za Ulaya na vita ya kushuka daraja.

Hizi hapa ni mechi zitakazopigwa leo:


Brentford vs Fulham

Saa 17:00
Dabi ya London Magharibi yenye ushindani mkali, timu zote zikisaka pointi muhimu kwa matumaini ya kumaliza juu ya msimamo.


Leeds United vs Wolverhampton Wanderers

Saa 17:00
Mchezo muhimu katika vita ya kujinusuru kushuka daraja, kila upande ukihitaji ushindi.


Newcastle United vs AFC Bournemouth

Saa 17:00
Newcastle wanataka kutumia uwanja wa nyumbani kupata pointi tatu, lakini Bournemouth wanaweza kushtukiza.


Tottenham Hotspur vs Brighton & Hove Albion

Saa 17:00
Tottenham wanapambana kujiweka salama, wakati Brighton wakisaka kuendeleza matokeo mazuri.


Chelsea vs Manchester United

Saa 19:30
Mchezo mkubwa wa siku ukipigwa Stamford Bridge, timu zote zikisaka ushindi muhimu katika mbio za kuwania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.