Goncalves afutwa kazi Yanga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th May 2026


Goncalves afutwa kazi Yanga

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Pedro Goncalves, raia wa Ureno.

Taarifa hiyo imetolewa muda mfupi baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC uliochezwa katika dimba la KMC Complex, ambapo Yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Licha ya kupata alama tatu muhimu, inaelezwa kuwa uongozi wa klabu haukuridhishwa na mwenendo wa timu kwa ujumla.

Katika mabadiliko hayo ya benchi la ufundi, Kocha Msaidizi Abdulhamid Moarin amepewa jukumu la kuiongoza timu akisaidiana na Patrick Mabedi hadi mwishoni mwa msimu.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha timu inaendelea kuwa katika ushindani huku klabu ikitafakari mustakabali wa benchi la ufundi.

Goncalves alijiunga na Yanga kwa matarajio makubwa, lakini matokeo na kiwango cha timu katika baadhi ya michezo yameonekana kuwa chini ya matarajio ya mashabiki na uongozi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.