Winga wa klabu ya Chelsea, Alejandro Garnacho, ametoa kauli kufuatia mjadala ulioibuka baada ya mahojiano ya hivi karibuni, akilenga moja kwa moja hali ya ndani ya kikosi cha Chelsea.
Garnacho amesema kuwa moja ya mambo makubwa aliyojifunza akiwa Manchester United ni umuhimu wa uwajibikaji wa wachezaji na uzalendo katika timu, akidai kuwa hilo linakosekana kwa kiasi kikubwa ndani ya Chelsea kwa sasa.
Ameongeza kuwa baadhi ya wachezaji wanapaswa kukomaa zaidi na kubeba majukumu yao badala ya kulaumiana au kujificha wanapokumbana na changamoto.
“Tazama, moja ya mambo makubwa niliyoyajifunza Manchester United ni kwamba uwajibikaji wa kweli kwa sasa unakosekana ndani ya dressing room ya Chelsea. Binafsi, ninaamini wachezaji wengi wanapaswa kukomaa na kuchukua majukumu zaidi badala ya kulaumiana au kujificha."
"Klabu inapitia kipindi kigumu, kila mtu anaona hilo, lakini huwezi kukimbia au kununa kila mambo yanapokwenda tofauti na matarajio. Hiyo hali ya kujiona bora inapaswa kukoma, inaidhoofisha timu. Hakuna mchezaji aliye mkubwa kuliko klabu. Si mimi, si mtu mwingine yeyote. Unapaswa kuheshimu nembo, unapaswa kumheshimu kocha, vinginevyo hustahili kuvaa jezi hiyo."



