Gamondi aongeza wawili Stars kutoka Serengeti Boys

Joel JJ By Joel JJ • 29th May 2026


Gamondi aongeza wawili Stars kutoka Serengeti Boys

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Miguel Gamondi, amewaongeza wachezaji wawili chipukizi kutoka timu ya taifa ya vijana ya chini ya miaka 17, maarufu kama Serengeti Boys, kwenye kikosi cha wakubwa cha Tanzania national football team.

Wachezaji waliopandishwa ni:

  • Luqman Mbalasu – Kiungo

  • Kassimu Juma – Mlinzi wa kushoto

Nyota hao wawili wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha Taifa Stars mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya AFCON U17 Final kati ya Serengeti Boys na Senegal  utakaochezwa Juni 02, 2026.

Hatua hiyo ya Gamondi ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuijenga upya Taifa Stars kwa kuwapa nafasi vijana wenye vipaji kuungana na wachezaji wenye uzoefu. 

Taifa Stars kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya michezo miwili muhimu ya kimataifa dhidi ya Uganda Juni 05, na kisha dhidi ya Rwanda Juni 09, mechi zote zikitarajiwa kuchezwa mjini Marrakech, Morocco.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.