Azam Fc imeendeleza wimbi la ushindi uwanja wa Azam Complex leo ikiichapa Namungo Fc bao 1-0 katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali.
Alikuwa ni Feisal Salum 'Fei Toto' aliyefunga bao pekee la Azam Fc kupitia mkwaju wa penati kwenye dakika ya 42 baada ya Japhet Kitambala kufanyiw madhambi ndani ya eneo la hatari.
Namungo Fc walikuwa na nafasi ya kurejea mchezoni lakini walipoteza nafasi adimu ya mkwaju wa penati kwenye kipindi cha pili
Fei Toto sasa amerejea juu kwenye mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 10, akiendeleza rekodi yake bora ya kufunga na kutoa pasi za mabao msimu huu.
Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' pia ni kinara wa pasi za mabao (8)



