Enzo aiwekea ngumu Chelsea, ataka kuondoka

Joel JJ By Joel JJ • 28th May 2026


Enzo aiwekea ngumu Chelsea, ataka kuondoka

Kiungo wa kimataifa wa Argentina, Enzo Fernández, ameweka wazi msimamo wake wa kutaka kuondoka katika klabu ya Chelsea FC katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi, huku mvutano kati ya pande hizo mbili ukizidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa za karibu, Chelsea imeweka dau kubwa la takribani pauni milioni 120 (zaidi ya shilingi bilioni 390) ili kumruhusu mchezaji huyo kuondoka, hatua inayoonyesha dhamira ya klabu kutotaka kumpoteza kwa bei ya chini.

Vilabu vikubwa Ulaya vamuandama

Hali ya Enzo imevuta hisia za mabingwa na vigogo wa soka barani Ulaya, ambapo klabu za Real Madrid, Manchester City na Paris Saint-Germain zimeanza kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25.

Vilabu hivyo vinaaminika kumwona Enzo kama kiungo muhimu anayeweza kuimarisha safu ya kati kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi, kudhibiti mchezo na kuchangia mabao.

Uhusiano na Chelsea wazidi kuzorota

Chanzo cha karibu kimeeleza kuwa uhusiano kati ya Enzo na Chelsea umeanza kuyumba, hasa baada ya mchezaji huyo kufungiwa mechi mbili mapema msimu huu kutokana na tukio lililotafsiriwa kama vitendo vya “kujipendekeza” kwa Real Madrid wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa mwezi Machi.

Tukio hilo limeongeza mvutano ndani ya klabu na kuchochea tetesi za kuhitaji mabadiliko ya mazingira kwa mchezaji huyo.

Mazungumzo ya mkataba yagonga mwamba

Mazungumzo ya kuongeza mkataba kati ya Chelsea FC na wakala wake, Javier Pastore, yameelezwa kugonga mwamba kutokana na Enzo kutoridhishwa na masuala ya mshahara pamoja na masharti ya kifedha yaliyowekwa na klabu.

Hali hii imeacha mlango wazi kwa klabu nyingine kuingia katika mbio za kumsajili.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.