Enzo Maresca ndiye mrithi wa Guardiola Man City

Joel JJ By Joel JJ • 26th May 2026


Enzo Maresca ndiye mrithi wa Guardiola Man City

Habari za moto na zimethibitishwa! Kocha wa zamani wa Chelsea, Enzo Maresca atajiunga na klabu ya Manchester City kuchukua nafasi ya Pep Guardiola.

Kwa mujibu wa mwanahabari maarufu wa usajili wa soka, Fabrizio Romano kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, amefichua taarifa za “EXCLUSIVE” zikidai kuwa Maresca tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu na Manchester City.

Romano ameandika kuwa makubaliano yote yamekamilika rasmi, na kwamba tangazo la Maresca kuwa kocha mpya wa City linatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kocha huyo anatajwa kuchukua nafasi ya Guardiola, ambaye ameiongoza City kupata mafanikio makubwa katika miaka 10, ikiwemo mataji ya Premier League na UEFA Champions League.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa Maresca amesaini mkataba unaoendelea hadi Juni 2029, hatua inayomaanisha kuwa klabu hiyo ya Etihad ina mpango wa muda mrefu wa kuendeleza falsafa yake ya soka la kumiliki mpira na mashambulizi ya kasi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.