Kocha wa England, Thomas Tuchel, ametangaza rasmi kikosi cha wachezaji 26 kitakachoiwakilisha England kwenye Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Marekani, Canada na Mexico.
Habari kubwa kwenye kikosi hicho ni kuachwa nje kwa beki Harry Maguire, ambaye alikuwa sehemu muhimu ya England katika mashindano makubwa ya nyuma. Maguire amesema amesikitishwa sana na uamuzi huo wa kuachwa nje ya kikosi.
Mbali na Maguire, nyota wengine walioachwa nje ni Phil Foden na Cole Palmer, huku mshambuliaji Ivan Toney akirejea kwenye kikosi baada ya kufanya vizuri katika ligi ya Saudi Arabia.
Kikosi kamili cha England – Kombe la Dunia 2026
Makipa
- Jordan Pickford
- Dean Henderson
- James Trafford
Mabeki
- Reece James
- Tino Livramento
- Nico O'Reilly
- John Stones
- Marc Guéhi
- Ezri Konsa
- Dan Burn
- Jarell Quansah
Viungo
- Declan Rice
- Jude Bellingham
- Jordan Henderson
- Kobbie Mainoo
- Elliot Anderson
- James Garner
- Eberechi Eze
- Morgan Rogers
Washambuliaji
- Harry Kane
- Ivan Toney
- Ollie Watkins
- Bukayo Saka
- Marcus Rashford
- Anthony Gordon
- Noni Madueke
Kundi la England Kombe la Dunia 2026
England imepangwa Kundi L pamoja na:
- Croatia
- Ghana
- Panama
England itaanza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa kucheza dhidi ya Croatia tarehe 17 Juni 2026 katika mechi ya ufunguzi ya kundi hilo.



