Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube jana aliendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu akifunga bao la kwanza wakati timu yake ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Bao hilo lilimfanya Dube afikishe mabao 9 sasa akilingana na kinara wa mabao Feisal Salum ambaye pia amefunga mabao 9.
Dube sasa amehusika katika mabao 13 ya Yanga akitoa pasi nne za mabao wakati Fei Toto akiongoza upande wa asisti pia akiwa nazo 8.
Dube amekuwa katika mwendelezo mzuri tangu alipopona majeruhi akiwa na wastani wa kufunga angalau bao moja katika kila mchezo.



