Dube, Ngoy wachuana ufungaji bora ligi kuu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st April 2026


Dube, Ngoy wachuana ufungaji bora ligi kuu

Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube anachuana vikali na mshambuliaji wa Namungo Fc Fabrice Ngoy wote wakifunga mabao nane kwenye ligi kuu ya NBC msimu huu.

Wakati Yanga ikiichapa Mbeya City mabao 6-0, Dube alifunga mabao mawili na hivyo kumfikia Ngoy ambaye amesimama kwenye mabao nane kwa muda mrefu.

Aidha nyota wengine wa Yanga Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua nao wako karibu na vinara hao wa mabao kila mmoja akifunga mabao 7.

Kiungo mshambuliaji wa Azam Fc Feisal Salum 'Fei Toto' nae ameweka kambani mabao saba pia akiwa kinara wa kutoa pasi za mabao ambapo anazo 7.

Feisal anaungana na nyota mwingine wa Azam Fc, winga Idd Nado ambaye pia amepachika mabao 7.

Katika orodha hiyo ya mabao 7 pia yumo kiungo mshambuliaji wa JKT Tanzania, Saleh karabaka anayeitumikia timu hiyo kwa mkopo akitokea klabu ya Simba.

Washambuliaji Laurindo Aurelio 'Depu' wa Yanga na Suleiman Mwalimu wa Simba wao wamepachika mabao 6 kila mmoja.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.