Kiungo wa kati wa Mali, Aliou Dieng, amekamilisha rasmi uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Hispania, Valencia CF akitokea klabu ya Misri Al Ahly SC
Dieng anatarajiwa kujiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya ya Valencia kuanzia Julai 6, ambapo ataanza rasmi mazoezi na wachezaji wenzake kuelekea msimu wa 2026/27.
Dieng ataanza mapema kuzoea mfumo wa timu mpya chini ya benchi la ufundi la Valencia, huku klabu hiyo ikimwona kama sehemu muhimu ya kuimarisha kiungo chake cha kati.
Uhamisho huo umekamilika baada ya Dieng kumaliza majukumu yake na Al Ahly, klabu aliyokuwa ameichezea kwa mafanikio makubwa barani Afrika.
Inaripotiwa kuwa makubaliano yake na Valencia yalifikiwa mapema, huku akitarajiwa kusaini mkataba wa muda mrefu kabla ya kuanza rasmi maisha yake ya soka barani Ulaya.
Dieng, ambaye anajulikana kwa uwezo wake wa kukaba, nguvu ya mwili na uchezaji wa kasi ya kurudisha mipira, anaingia Valencia kama mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kuongeza uimara katika eneo la kiungo.



