Da Cruz Kocha Mpya Kaizer Chiefs

Joel JJ By Joel JJ β€’ 1st June 2026


Da Cruz Kocha Mpya Kaizer Chiefs

Klabu ya Kaize Chiefs ya Afrika Kusini, imemteua kocha Mfaransa, Fernando Da Cruz, kuwa meneja mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa za karibu na klabu, Da Cruz amekamilisha makubaliano na uongozi wa Kaizer Chiefs na kusaini mkataba huo mpya unaomuweka rasmi kama mrithi wa majukumu ya kuiongoza timu hiyo katika msimu ujao.

Kocha huyo wa zamani wa Lille OSC na pia aliyewahi kufanya kazi na AS FAR Rabat, anatarajiwa kuwasili akiwa na timu yake ya wasaidizi wanne, huku pia wakiunganishwa na makocha 2–3 wa Afrika Kusini ili kusaidia mchakato wa ujenzi wa kikosi.

Uongozi wa Kaizer Chiefs umeonekana kuwa katika hatua ya kujenga upya timu ili kurudisha makali yao kwenye ligi ya Afrika Kusini baada ya misimu ya matokeo yasiyoridhisha.

Ujio wa Da Cruz unaashiria mwelekeo mpya wa kimkakati, ambapo klabu hiyo inatarajia kutumia uzoefu wake wa kimataifa kuimarisha nidhamu ya kiufundi, mbinu za kisasa za soka na ushindani katika ligi na mashindano ya Kimaataifa.

Msimu uliopita Chiefs ilinolewa na makocha vijana Cedric Kaze na Ben Youssef ambao walichukua majukumu yaliyoachwa na aliyekuwa kocha mkuu Nasreddine Nabi ambaye aliondoka kutokana na changamoto za kifamilia.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.