Coastal Union yapania alama tatu dhidi ya Simba

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th May 2026


Coastal Union yapania alama tatu dhidi ya Simba

Kuna dakika 180 zitapigwa kati ya Simba dhidi ya Coastal Union maarufu wagosi wa Kaya. Kabla ya timu hizo kukutana kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB, Alhamisi May 21 zitakutana kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Coastal Union watakuwa wenyeji wa mchezo huo wa ligi ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Wakipambana kujiweka katika nafasi nzuri ili kuepuka kushuka daraja, Coastal Union wametamba kuchukua alama tatu.

Mapema tu wametangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa saa 12 jioni.

Hata hivyo haitakuwa kazi rahisi mbele ya kikosi cha Simba kinachonolewa na kocha Steve Barker ambaye ni kama ameshajipata.

Barker hajapoteza mchezo wowote wa ligi tangu alipoanza kuinoa Simba mwishoni mwa Disemba 2025.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.