Bayern, Arsenal mguu ndani nusu fainali UEFA

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 8th April 2026


Bayern, Arsenal mguu ndani nusu fainali UEFA

Matokeo ya michezo ya robo fainali mkondo wa kwanza wa UEFA Champions League yaliyochezwa usiku wa leo:

• Real Madrid 1–2 Bayern Munich

Mchezo huu uliokuwa na ushindani mkubwa umemalizika kwa Bayern Munich kuibuka na ushindi muhimu ugenini. Mabao ya Luis Díaz na Harry Kane ndio yaliyozamisha jahazi la Los blancos huku bao pekee la kufutia machozi likifungwa na Kylian Mbappé na kuhakikisha Bayern wanachukua ushindi huo muhimu kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa Allianz arena (Ujerumani).

• Sporting CP 0–1 Arsenal

Arsenal wamefanikiwa kupata ushindi mwembamba ugenini kupitia bao pekee la dakika za jioni la Kai Havertz, matokeo yanayowaweka katika nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano pale Emirates stadium (uingereza).

Kwa matokeo haya, Bayern Munich na Arsenal wanaondoka na faida muhimu, huku Real Madrid na Sporting CP wakilazimika kupambana zaidi katika michezo ya marudiano ili kugeuza matokeo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.