Barcelona waiomba Uefa kukagua uwanja metropolitano

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 14th April 2026


Barcelona waiomba Uefa kukagua uwanja metropolitano

Klabu ya FC Barcelona imewasilisha ombi rasmi kwa UEFA ikiitaka ifanye ukaguzi wa uwanja wa Estadio Metropolitano, unaotumiwa na Atlético Madrid, kufuatia wasiwasi kuhusu hali ya nyasi.

Kwa mujibu wa Barcelona, nyasi za uwanjani humo zinadaiwa kuwa ndefu kupita kiwango kinachokubalika, hali ambayo inaweza kuathiri mtindo wao wa kucheza mpira wa pasi za chini. Klabu hiyo imesisitiza kuwa UEFA ndiyo mamlaka yenye jukumu la kuhakikisha kunakuwepo usawa na haki kwa pande zote, hivyo kuomba hatua zichukuliwe mapema kabla ya mchezo husika.

Hata hivyo, Atlético Madrid wamekanusha madai hayo wakieleza kuwa uwanja uko katika hali ya kawaida na hauhitaji ukaguzi wowote wa ziada. Wenyeji hao wamesisitiza kuwa nyasi ipo katika kiwango kinachotumika mara kwa mara bila tatizo lolote.

Kwa sasa, uamuzi wa mwisho uko mikononi mwa UEFA, ambao wanatarajiwa kuamua iwapo watafanya ukaguzi rasmi au watakataa ombi hilo. Sakata hili limeongeza mvutano kuelekea mechi hiyo muhimu, huku pande zote zikiendelea kusimamia misimamo yao.

Chanzo; @Marca


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.