Azam Fc yaichapa Mashujaa Fc 1-0, yatinga nusu fainali CRDB Cup

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th May 2026


Azam Fc yaichapa Mashujaa Fc 1-0, yatinga nusu fainali CRDB Cup

Azam Fc imetinga robo fainali ya kombe la CRDB baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Bao la mpira wa adhabu lililofungwa na Idi Nado lilitosha kuihakikishia Azam Fc ushindi muhimu katika mchezo ambao wauza Ice cream hao walitawala kwa muda mwingi hasa kipindi cha kwanza.

Ni rasmi sasa Azam Fc watamenyana na Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali.

Tayari timu tatu zimefuzu nusu fainali ambazo ni Coastal Union, Yanga na Azam Fc.

Mchezo wa kuhitimisha hatua ya robo fainali unazikutanisha Simba dhidi ya TRA United ukipigwa dimba la KMC Complex.

Mshindi wa mchezo huo atachuana na Coastal Union hatua ya nusu fainali.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.