Azam Fc kumuongeza mkataba Mao

Joel JJ By Joel JJ β€’ 29th May 2026


Azam Fc kumuongeza mkataba Mao

Klabu ya Azam Fc imefungua mazungumzo na kiungo mkongwe Himid Mao ili kuhuisha mkataba wake unaoelekea ukingoni.

Mao ambaye alirejea Azam FC baada ya kucheza soka la kulipwa nchini Misri kwa miaka kadhaa, ameonekana kuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.

Uzoefu wake mkubwa pamoja na uwezo wa kuiongoza timu katikati ya uwanja vimeifanya benchi la ufundi kuona umuhimu wa kuendelea kubaki naye kwa muda mrefu zaidi.

Inaelezwa kuwa tayari viongozi wa Azam wameanza mazungumzo ya awali na kiungo huyo ili kuhakikisha anasaini mkataba mpya kabla ya timu nyingine kuanza kuonyesha nia ya kumhitaji.

Tangu arejee ndani ya kikosi hicho, Mao ameonyesha utulivu mkubwa uwanjani huku akiwa mmoja wa wachezaji wanaobeba falsafa ya timu.

Mbali na ubora wake wa kucheza, Mao pia amekuwa msaada mkubwa kwa wachezaji vijana ndani ya kikosi hicho kutokana na uzoefu alioupata nje ya nchi akiwa kwenye ligi ya Misri. Hilo limeongeza thamani yake ndani ya timu na kuwafanya viongozi kuona bado ana mchango mkubwa kwa siku zijazo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.