Azam Fc ilivyoitunishia misuli Mali

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th June 2026


Azam Fc ilivyoitunishia misuli Mali

Kocha Florent Ibenge ataendelea kusalia Azam Fc kwa mwaka mmoja zaidi baada ya kuongeza mkataba utakaomuweka viunga vya Chamazi hadi mwaka 2028.

Klabu ya Azam Fc methibitisha rasmi kumuongeza mkataba kocha huyo Mcongomani aliyejijengea heshima ya kipekee kwenye soka la Afrika.

Ibenge alikuwa tayari amefikia makubaliano na Shirikisho la soka la Mali kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa. Hata hivyo Ibenge akajiondoa kwenye mchakato licha ya kuwa tayari alishapitishwa.

Ni baada ya Azam Fc 'kupiga comeback' iliyomshawishi kuongeza mwaka mwingine ili kuendelea na project ya kuisuka Azam Fc aliyoanza msimu huu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.