Azam Fc bado haijakata tamaa na Ebuela

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th April 2026


Azam Fc bado haijakata tamaa na Ebuela

Klabu ya Azam FC ya Tanzania inaripotiwa kuendelea kumfuatilia beki wa kulia raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Steve Ebuela, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Al Hilal SC, katika jitihada za kuimarisha safu yake ya ulinzi kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa taarifa za karibu na uongozi wa klabu hiyo, Azam FC iliwahi kujaribu kumsajili mchezaji huyo katika dirisha lililopita la usajili, lakini mazungumzo hayakufikia makubaliano ya mwisho kutokana na changamoto za kimkataba na muda wa uhamisho.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo imerejea tena katika mpango wa kumtaka beki huyo, ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliopendekezwa na kocha Florent Ibenge.

Inasemekana Ibenge anamuhitaji Ebuela kwa kuwa alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi chake wakati wote wawili hao walipokuwa wakifanya kazi katika klabu ya Al Hilal, ambapo beki huyo alionesha uwezo wake katika nafasi ya ulinzi wa pembeni.

Ebuela, ambaye anacheza kama beki wa kulia, anasifika kwa kasi, uwezo wa kusaidia mashambulizi pamoja na nidhamu ya kiulinzi, sifa ambazo zinaonekana kuendana na mahitaji ya Azam FC katika kuimarisha kikosi chake.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.