Arsenal yachapika Etihad, Mbio za ubingwa EPL ni kama zimeanza upya

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 19th April 2026


Arsenal yachapika Etihad, Mbio za ubingwa EPL ni kama zimeanza upya

Klabu ya Manchester City imeibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Premier League uliochezwa katika dimba la Etihad, matokeo yaliyoitikisa kwa kiasi kikubwa mbio za ubingwa wa msimu huu.

Katika mchezo huo, City walipata mabao kupitia Rayan Cherki na Erling Haaland, huku bao la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Kai Havertz.

Ushindi huo unaongeza presha kwa Arsenal, ambao wamekuwa wakiongoza ligi kwa muda mrefu lakini sasa wanaonyesha dalili za kushuka kiwango. Katika michezo sita ya hivi karibuni, Gunners wameshinda mara moja pekee na kupoteza mara nne hali inayotia shaka juu ya uwezo wao wa kudumisha ubora hadi mwisho wa msimu.

Kwa upande wa Manchester City, ushindi huo unawapa nguvu mpya katika mbio za ubingwa, huku wakibaki na mechi nyingi zaidi ya Arsenal hali inayoweza kuwapa faida muhimu katika wiki za mwisho za ligi.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, ameendelea kusisitiza kuwa mbio za ubingwa bado hazijaamuliwa, akieleza kuwa timu yake bado inaongoza kwa tofauti ya pointi na kuna mechi kadhaa muhimu zilizosalia.

Hata hivyo, matokeo ya mchezo huo yamebadilisha mwelekeo wa ushindani, huku Manchester City wakionekana kuimarika zaidi katika kipindi hiki muhimu cha msimu.

Kwa sasa, mbio za ubingwa wa Premier League zinaingia katika hatua ya mwisho yenye ushindani mkali, ambapo kila pointi inaweza kuamua nani atakayenyanyua taji mwishoni mwa msimu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.