Ancelotti aongeza minne Brazil

Joel JJ By Joel JJ • 15th May 2026


Ancelotti aongeza minne Brazil

Shirikisho la Kandanda la Brazil (Confederação Brasileira de Futebol) limetangaza rasmi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, amesaini mkataba mpya wa miaka minne utakaomuweka katika nafasi hiyo hadi Julai 2030.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makubaliano hayo mapya yanakuja baada ya CBF kuridhishwa na mwelekeo wa kiufundi wa kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Ulaya, na sasa atakuwa na jukumu la kuongoza moja ya mataifa yenye historia kubwa ya mafanikio katika soka la dunia, Brazil.

Awali, Ancelotti alitarajiwa kumaliza mkataba wake baada ya Kombe la Dunia la 2026, lakini sasa makubaliano mapya yanamaanisha ataendelea kuinoa Brazil katika mashindano mawili makubwa ya Kombe la Dunia 2026 na 2030 ikiwa ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuirejesha timu hiyo kileleni mwa soka la kimataifa.

CBF imesema kuwa uamuzi huo unalenga kuhakikisha uthabiti wa kikosi na falsafa ya muda mrefu, hasa katika kipindi ambacho Brazil imekuwa ikifanya mabadiliko ya kiufundi na kujaribu kujenga kizazi kipya cha wachezaji.

Ancelotti, ambaye amewahi kufundisha vilabu vikubwa barani Ulaya na kushinda mataji mbalimbali ya ndani na ya kimataifa, anatarajiwa kutumia uzoefu wake kuunganisha vipaji chipukizi na wachezaji wenye uzoefu katika kikosi cha Brazil.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.