Aliou Cisse kuinoa Angola

Joel JJ By Joel JJ • 9th April 2026


Aliou Cisse kuinoa Angola

Shirikisho la Kandanda la Angola (FAF), limekamilisha mazungumzo na kocha Aliou Cissé kutoka Senegal wakimteua kuwa kocha mpya wa timu yao ya taifa, Palancas Negras.

Cissé, ambaye aliongoza timu ya taifa ya Senegal kufikia mafanikio makubwa ikiwemo kufika fainali ya Kombe la Afrika (AFCON) 2021, tayari amekubali kuinoa Angola.

Taarifa kutoka kwa vyanzo vya karibu na shirikisho la kandanda la Angola zinaonyesha kuwa kocha huyo anatarajiwa kuchukua mikoba ya timu hiyo katika hatua za mashindano ya kimataifa.

Cissé anakuja akiwa na uzoefu mkubwa wa kuiongoza timu za taifa, pamoja na safari yake ya hivi karibuni akiwa kocha wa Libya, ambapo aliondoka kutokana na changamoto za kifedha na mkataba.

Mashabiki wa Palancas Negras na wadau wa soka nchini Angola wanatarajia uteuzi wa Cissé uanze kutekelezwa haraka, wakiamini kwamba kocha huyo mwenye uzoefu wa kimataifa atasaidia kuongeza ushindani wa timu ya taifa ya Angola.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.