Timu ya Aigle Noir CS imetawazwa rasmi kuwa Bingwa wa Ligue A Burundi Msimu wa 2025-2026 katika Sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa NPPC.
Aigle Noir, wanaojulikana pia kama “The Fighters”, walihitimisha Msimu wakiwa na pointi 71, idadi sawa ya alama walizokuwa nazo walipotwaa Ubingwa msimu uliopita.
Mbali na kunyanyua Kombe la Ligi Kuu, Mabingwa hao pia walikabidhiwa zawadi ya fedha taslimu kiasi cha faranga Milioni 50 za Burundi kutokana na mafanikio yao ya msimu huu.
Ubingwa huo unaendelea kuthibitisha ubora wa Aigle Noir CS katika soka la Burundi baada ya kuendelea kutawala Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo.



