Ivory Coast yaipa Afrika ushindi wa kwanza Kombe la Dunia 2026, Sweden yaichapa Tunisia 5-1

Joel JJ By Joel JJ • 15th June 2026


Ivory Coast yaipa Afrika ushindi wa kwanza Kombe la Dunia 2026, Sweden yaichapa Tunisia 5-1

Bara la Afrika limepata ushindi wake wa kwanza katika Kombe la Dunia 2026 baada ya Ivory Coast kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ecuador katika mchezo wa Kundi E uliochezwa Jumapili usiku.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na nyota wa Manchester United Amad Diallo limetosha kuwapa Ivory Coast pointi tatu muhimu na kuifanya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kuonja ladha ya ushindi katika mashindano hayo yanayoendelea nchini Marekani, Canada na Mexico.

Ushindi huo umewapa Wana Tembo matumaini makubwa ya kufuzu hatua ya 32 bora, hasa baada ya matokeo mengine ya kundi hilo kushuhudia Ujerumani ikiifunga Curaçao mabao 7-1 na kuongoza kundi kwa tofauti kubwa ya mabao.

Kocha wa Ivory Coast Emerse Fae aliisifu timu yake kwa nidhamu ya mchezo na uwezo wa kuhimili presha kutoka kwa Ecuador katika dakika za mwisho za mchezo.

Wakati huo huo, matumaini ya Tunisia yalianza vibaya baada ya kupokea kichapo kikubwa cha mabao 5-1 kutoka Sweden katika mchezo wa Kundi F.

Sweden ilionyesha ubora mkubwa tangu mwanzo wa mchezo na kufunga mabao matatu kabla ya mapumziko, jambo lililoifanya Tunisia kushindwa kurejea mchezoni licha ya kupata bao la kufutia machozi katika kipindi cha pili.

Matokeo hayo yanaifanya Sweden kuanza kampeni yake kwa kishindo na kujikita katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, huku Tunisia ikilazimika kutafuta matokeo mazuri katika michezo yake ijayo ili kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu hatua inayofuata.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.