Simba yafuata beki TP Mazembe

Joel JJ By Joel JJ β€’ 14th June 2026


Simba yafuata beki TP Mazembe

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imeingia kwenye mchakato wa mazungumzo ya kumsajili beki na nahodha wa TP Mazembe, Madou Zon (27), katika juhudi za kuimarisha safu yao ya ulinzi kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa, Simba SC wameonyesha nia ya dhati ya kumleta nyota huyo kutoka DR Congo, ambaye kwa sasa ndiye mmoja wa mabeki wanao-zungumzwa zaidi katika Ligi ya Congo.

Zon amekuwa katika kiwango bora msimu huu, ambapo alitajwa kuwa MVP wa duru la kwanza la ligi ya Congo DR, na bado ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya MVP wa msimu kutokana na ubora wake.

Uimara wake katika ulinzi, uwezo wa kuongoza wenzake, pamoja na uzoefu wake katika mechi kubwa, vimefanya aendelee kuvutia vilabu kadhaa barani Afrika.

Kocha wa Simba SC Steve Barkrer anaripotiwa kuwataka viongozi wa Simba kumaliza dili hilo haraka, akiamini Zon anaweza kuwa nguzo muhimu kwenye ulinzi na msaada mkubwa katika mashindano ya CAF.

Licha ya Ismail Toure kuendelea kufanya vyema akishirikiana na Rushine De Reuck ujio wa Zon utamuongezea Barker machaguo katika eneo hilo muhimu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.