Yanga mikononi mwa Mashujaa Fc Kigoma, mechi tatu kupigwa leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th June 2026


Yanga mikononi mwa Mashujaa Fc Kigoma, mechi tatu kupigwa leo

Mabingwa watetezi ligi kuu ya NBC Yanga leo wako mkoani Kigoma kumenyana na Mashujaa Fc katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC raundi ya 26.

Ni mechi za lala salama, kila timu ikihitaji alama tatu muhimu ili kutimiza malengo yake ya msimu huu.

Kwa Yanga ni mchezo ambao wanahitaji ushindi ili kuendelea kujiweka katika mazngira mazuri ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

Wananchi wanafahamu matokeo tofauti na ushindi yatawaweka katika presha kubwa hasa wakizingatia watani zao Simba wako karibu yao na wao watashuka dimba la KMC hapo kesho kuikabili Pamba Jiji.

Mchezo wa mapema saa 8 Mbeya City watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar uwanja wa Sokoine katika mchezo ambao Mbeya City inahitaji ushindi ili kuweka hai matumaini yao ya kusalia ligi kuu.

JKT Tanzania na Singida BS zitachuana katika mchezo mwingine wa vita ya kuwana nafasi ya nne.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.