Baada ya takribani wiki mbili za mapumziko ya kalenda ya FIFA, Ligi Kuu ya NBC inarejea leo mzunguuko wa 26 kwa mechi tatu kupigwa.
Fountain Gate watakuwa wenyeji wa Azam Fc mchezo utakaopigwa saa 10 uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha wakati Coastal Union wakiwakaribisha Namungo Fc katika mchezo mwingine utakaokuwa unapigwa muda huo kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Mchezo utakaohitimisha ratiba ya leo ni kati ya KMC dhidi ya TRA United uwanja wa KMC Complex.




