Rice ateuliwa Makamu Nahodha wa England kuelekea kombe la Dunia 2026

Joel JJ By Joel JJ • 8th June 2026


Rice ateuliwa Makamu Nahodha wa England kuelekea kombe la Dunia 2026

Kiungo wa Arsenal FC na timu ya taifa ya England, Declan Rice, amepewa jukumu jipya la uongozi baada ya kuteuliwa kuwa makamu nahodha wa timu hiyo kuelekea Kombe la Dunia la 2026.

Uthibitisho huo umetolewa na kocha mkuu wa England, Thomas Tuchel, ambaye amesema Rice atakuwa msaidizi mkuu wa nahodha katika kikosi chake kipya.

“Kuanzia leo, Declan Rice ndiye makamu nahodha wangu,” alisema Tuchel akionyesha imani kubwa kwa kiungo huyo ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa England katika miaka ya karibuni.

Uamuzi huo unakuja baada ya Rice kuwa na msimu bora akiwa Arsenal, ambapo ameendelea kuthibitisha ubora wake kama mmoja wa viungo bora barani Ulaya. Mbali na mchango wake wa kiuchezaji, Rice ameonyesha sifa za uongozi, utulivu na uwezo wa kuhamasisha wenzake ndani na nje ya uwanja.

Katika msimu uliomalizika, nyota huyo alihusika moja kwa moja katika mabao 16 kupitia kufunga na kutoa pasi za mabao, huku akiendelea kuwa nguzo muhimu katika safu ya kiungo ya Arsenal na timu ya taifa ya England.

Tangu aanze kuitumikia England, Rice amekuwa mmoja wa wachezaji wanaoaminika zaidi kutokana na uwezo wake wa kulinda safu ya ulinzi, kuanzisha mashambulizi na kusimamia tempo ya mchezo. Sasa majukumu yake yataongezeka baada ya kupewa nafasi ya kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa kikosi hicho.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.